The United Republic of Tanzania Ministry of Health Southern Zonal Referral Hospital

Media Center

KIKAO CHA WATUMISHI WOTE KILICHOLENGA MABORESHO MAKUBWA YA HUDUMA HOSPITALI YA RUFAA KANDA YA KUSINI-MTWARA

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini Dkt. Herbert Masigati ameongoza kikao Cha Watumishi wote kilicholenga zaidi kujadili njia mbalimbali za kuboresha huduma zinazotolewa ili kuendelea kuhudumia wananchi.

Dkt. Masigati ametoa wito kwa watumishi hao kufanya kazi kwa weledi kwa kizingatia Sheria, Taratibu, kanuni na miongozo iliyowekwa na Wizara ya afya hali itakayopelekea huduma hospitalini hapo kuwa Bora zaidi.


Kupitia kikao hicho watumishi mbalimbali walipata nafasi ya kutoa mawazo ya jinsi ya kuboresha huduma na kuwavutia wateja wengi kuja kupata huduma hospitalini hapo ikiwa ni pamoja na uwekaji wa kambi za matibabau, ununuzi wa vifaa tiba kwenye vitengo mbalimbali kama vile macho, radiolojia, pamoja na kuongeza matangazo kuhusu huduma zinazotolewa katika hospitali hiyo.